Habari

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema anaunga mkono azima ya Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hasaan Joho kuwania wadhfa wa urais kwa Tiketi ya chama Cha Odm mwaka 2022.

Akizungumza mjini voi Raila amesema gavana Joho anahaki kikatiba na kama mwanachama wa chama hicho kuwania wadhfa huo wa urais.

Awali gavana Joho alinikuliwa akisema kwa muda wamekuwa wakiunga mkono viongozi wengine na sasa ni zamu yake kuungwa mkono.

Raila anatarajiwa kuongoza mikutano kadhaa ya hadhara katika maeneo mbalimbali Kaunti hiyo ya Taita Kabla ya kutamatisha ziara yake ya siku mbili Katika Kaunti hiyo.