HabariKimataifa

Hayati John Pombe Magufuli kuzikwa alhamisi wiki ijayo…

Hayati John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzikwa siku ya alhamisi wiki ijayo ambayo ni tarehe 25 ya mwezi huu.

Akitoa ratiba ya mazishi, Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema taifa la Tanzania litakuwa katika kipindi cha maombolezi kwa siku 21.

Tarehe 20 siku ya Jumamosi mwili wa Magufuli utatolewa katika hospitali ya jeshi na kupelekwa katika uwanja wa uhuru ili kuagwa na viongozi. Tarehe 21 wananchi watauaga mwili kisha usafirishwe hadi jijini Dodoma.

Tarehe 22 itakuwa siku ya mapumziko Tanzania mwili wake ukiagwa rasmi Dodoma. Tarehe 23 mwili wake utaagwa Mwanza na baadaye kusafirishwa kuelekea Chato ambapo wakaazi wake watauaga mwili wa mwendazake tarehe 24.

Shughuli za mazishi zitafanyika tarehe 25 huko nyumbani kwake Chato baada ya ibada katika kanisa katoliki siku hiyo aidha itakuwa siku ya mapumziko.