AfyaHabariKimataifa

Shirika la afya duniani WHO latoa wito kwa makampuni ya kutengeneza chanjo dhidi ya corona kwa mataifa yaliyoendelea kusaidia kusambaza kwa dharura dozi milioni 10 kupitia mpango wa covax ili kuyanufaisha mataifa maskini.

Mkurugenzi wa  WHO tedros  amesema mwaka ulipoanza alitoa hakikisho kwamba katika kipindi cha siku mia 100 duniani kila taifa litakua limeanza kutoa chanjo kwa raia wake. Tedros  amesema kwamba siku zimesalia 15  kwa kipindi hicho kukamilika  huku mataifa 16 yakiwa hayajatoa chanjo hiyo.

Miongoni mwa maitaifa hayo 16 yanatarajiwa kuanza kupokea chanjo hiyo juma lijalo huku 20 yakiwa hayana mpango wowote  wa kupata chanjo.Mkurugenzi huyo amesema kwamba mpango wa covax  utayari kusambaza chanjo kwa mataifa yote maskn ila chanjo hiyo haipatikani.

Covax inalenga kusambaza chanjo milioni mbili kwa mataifa hayo katkia kipindi cha mwaka mmoja  huku akiwashtumu mataifa tajiri kwa kujinunulia chanjo nyingi hivyo kusababisha nchi nyingine kukosa. ni wiki hii   ambapo taifa la india lilitangaza kusitisha kwa muda usambazaji wa  chanjo ya astrazeneca kufuatia ongezeko la maambukizi nchini humo uamuzi ambao WHO umeielewa.

Kulingana na repoti ya hivi punde ya WHO iliyotolewa siku ya jumanne  ,Marekani inaongoza kwa utoaji chanjo  ambapo asilimia 39 ya raia wake wamechanjwa  ikifiuatwa na mataifa ya bara uropa ambapo wamechanja asilimia 14  na bara la  afrika ikisalia nyuma kabisa ambapo idadi ya waliochanjwa ni asilimia 0.68.