AfyaHabariWorld

Maafisa wa usalama wa Vikosi vya KDF walioko nchini Somalia wapokea dozi yao ya kwanza ya Covid-19…………

Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu katika Jeshi la Ulinzi la Kenya Meja jenerali George Ng’ang’a, amezindua zoezi la chanjo hio kwa wanajeshi waliopelekwa nchini humo  chini ya mpango wa Umoja wa Afrika katika Makao Makuu ya Sekta ya II mjini Dhobley .

Hii ni Awamu ya kwanza inayoendelea ya Mpango wa Taifa katika harakati za kukabiliana na janga la Covid-19.

Ng’ang’a amewataka watumishi wote kushiriki katika zoezi la kinga ili kuongeza juhudi za kupambana na janga hilo.