AfyaHabariLifestyle

UCHAFUZI WA MAZINGIRA WAZIDI KUWA KERO MALINDI

Wakaazi mjini malindi kaunti ya kilifi wameombwa kukoma kuweka taka kwenye mabomba yakupitisha maji taka na badala yake kutupa taka hizo kwa maeneo yaliyotengwa na Serikali ya Kaunti.

Mhandisi Nicodemus Kerongo ambaye ni Afisa wa Kaunti ya Kilifi katika kitengo cha Barabara na usafi mjini humo, anasema Wakaazi wamekuwa na tabia ya kutupa taka ovyo katika mabomba hayo na kuzuia njia ya maji machafu.

Akizungumza Afisini mwake Kerongo amedai hatua hiyo imesababisha baadhi ya wafanyikazi wake kuambukizwa maradhi wakati wanapokuwa kazini kusafisha uvundo wa taka hizo.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Kaunti hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha swala hilo linashughulikiwa ipasavyo.

Kerongo amedokeza kuwa tayari wameajiri jumla ya vijana 33 kutoka maeneo bunge ya Magarini na Malindi mtawalia ili kuendeleza juhudi za kusafisha mabomba ya maji taka.