HabariMombasa

WAKENYA WAHIMIZWA KUZINGATIA MASHARTI YA COVID 19.

Mbunge wa Mvita kaunti ya Mombasa Abhulswamad Sharif, amewataka Wakenya kuendelea  kufuata sheria zilizowekwa na wizara ya afya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona

Abhulswamad amewataka wakaazi kuendelea kutii maagizo yaliotolewa na rais Uhuru Kenyatta kwenye hotuba yake alioitoa kwa taifa ijumaa iliopita kuhusiana na janga la corona.

Mbunge huyo amesema itakuwa si jambo la busara kwa wananchi kuwakashifu viongozi kutokana na maagizo hayo yaliotolewa na serikali.

Abdhulswamad amabaye tayari amechanjwa chanjo hio ya kukabiliana na covid-19, ametoa wito kwa wakaazi hao kujitokeza kwa wingi kuchanjwa huku akishikililia kwamba chanjo hio ni salama kwa binadamu.