Habari

MASENETA WAKOSOA ZOEZI LA USAJILI WA MAKURUTU.

Maseneta sasa wanashinikiza serikali kufutilia mbali zoezi la usajili wa makurutu kujiunga na jeshi KDF.

Maseneta hao akiwepo Ledama Olekina wa Narok wanadai zoezi hilo lilikumbwa na visa vya udanganyifu na ulaji rushwa na hivyo linapaswa kufanya upya.

Olekina amelaumu tume ya maadili na kukabili ufisadi kwa kushindwa kuzuia visa hivyo.

Hata hivyo KDF imepinga madai hayo ikisema visa vilivyo ripotiwa wakati wa zoezi hilo la mwezi uliopita vilishugulikiwa ipasavyo.