HabariKimataifa

Rais Kenyatta amuomboleza mwanamfalme Philip wa Uingereza…

Rais Uhuru Kenyatta amejiunga na viongozi wengine wa ulimwengu kumuomboleza Prince Philip, mwanamfalme wa Edinburg aliyefariki hii leo.

Prince Philip, mwenye umri wa miaka 99, alikuwa mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza na mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia ya Uingereza.

Katika ujumbe wake wa rambirambi kwa Mfalme wake Malkia Elizabeth II,Rais Kenyatta amesema kuwa Mtawala wa Edinburg amekuwa mtu anayeunganisha ulimwengu.

Rais amesema amepokea habari za kifo cha Prince Philip kwa huzuni kubwa akisema wakenya na Serikali ya Kenya wanaungana na Familia ya Kifalme, Uingereza na ulimwengu kuomboleza Mfalme aliyeondoka.