AfyaHabariSiasa

Naibu rais atetea uamuzi wake wa kudungw chanjo ya Sputnik V…

Naibu wa Rais William Ruto ametetea uamuzi wake wa kupendelea chanjo dhidi ya Corona ya Sputnik V badala ya chanjo ya Astrazeneca ambayo Rais Uhuru na mawaziri wengi waliyopokea.

Katika mahojiano ya kipekee na runinga moja humu nchini,  Ruto amesema a hakualikwa katika kikao hicho na mawziri cha kupokea chanjo hiyo  dhidi Corona ya Astrazeneca iliyofanyika katika ikulu mnamo Machi tarehe 26 mwaka huu, Jambo lililompelekea kulipia chanjo ya Sputnik V kwa shilingi 7000.

Aidha amesema serikali haikuchagua chanjo ambayo mawaziri walifaa kudungwa, hatua ambayo ilifanya mawaziri hao kudungwa chanjo ya Astrazeneca iliyokuwepo wakati huo.

Wakati huo huo Ruto amepinga kauli ya serikali ya kusitisha chanjo hiyo ya Sputnik V  katika hospitali za kibinafsi, akisema hospitali hizo zingezidi kuhimizwa kupeana chanjo hiyo kwani kuna wakenya kama yeye wanaoweza kulipia chanjo hiyo.

Ameongezea hatua hii itaweza kufungua uchumi wa nchi ambao umezidi kuenda chini kutokatana na janga la Corona.