HabariSiasa

Tume ya Huduma za Mahakama JSC kusubiri uamuzi wa Mahakama kabla ya kutoa ripoti

Tume ya Huduma za Mahakama JSC imesema kuwa itasubiri  uamuzi wa Mahakama kabla ya kutoa ripoti yake kuhusu mahojiano ya kumatfuta Jaji Mkuu ambayo yamekamilika hii leo.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Profesa Olive Mugenda amesema kwamba shughuli ya kuandaa ripoti haitaendeela jinsi ilivyopangwa hadi rufaa walioyowasilisha itakaposikilizwa na kuamuliwa..

Hata hivyo siku ya Jumatano mahakama Kuu iliagiza kusitishwa kwa mchakato wa kuendelea kumtafuta jaji Mkuu kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani kupinga shughuli hiyo.

Uamuzi huo aidha ulisitisha shughuli ya kuwahoji watu wanaotafuta nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Juu iliyoratibiwa kuanza Jumatatu juma lijalo.

By: News Desk