Habari

Wanaume wawili wakamatwa Nairobi na pesa bandia…

Wanaume wawili wanaendelea kuhojiwa na polisi baada ya kukamatwa jana usiku huko Nairobi wakiwa na pesa bandia zenye thamani ya shilingi milioni 750.

Wawili hao ambao wametambulika kama Samuel Maina na Bonface Mungai walikamatwa katika nyumba moja eneo la Kilimani na pesa hizo bandia ambazo zilikuwa zimepakiwa katika masanduku.

Wakati wa msako huo polisi pia walipata kemikali zinazotumika kuchapisha pesa hizo pamoja na vitambulisho bandia vya umoja wa mataifa, wizara ya fedha pamoja na kampuni moja.

Aidha mkuu wa polisi Nairobi Augustine Nthumbi amesema bado uchunguzi unaendelea kubaini iwapo pesa hizo zimesambazwa sehemu mbalimbali.

By Aisha Juma