HabariSiasa

Kinara Wa The Service Party Mwangi Kiunjuri aapa kuendeleza Kampeni za BBI………..

Kinara wa chama cha The Service Party Mwangi Kiunjuri ameapa kuendeleza  kampeini za kupinga mchakato wa katiba kufanyiwa marekebisho kupitia mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Mwangi aliyekuwa waziri wa kilimo amesema kuwa mswada huo una dosari nyingi jambo ambalo limesababisha mivutano baina ya wabunge na maseneta.

Aidha amesema mswada haujaangazia maswala ya mwananchi wa kawaida na unawalenga tu kuwanufaisha watu wachache serikalini huku wakenya wengi wakizidi kuumia na mzigo wa kodi.

Ameongezea kwamba pendekezo la kubuni maeneo bunge mapya 70  kwenye  BBI kunazua mkanganyiko wa kisheria  na wakaazi wa mlima Kenya watazidi kupinga mchakato huo iwapo haitazingatia jinsi itakavyowanufaisha.

By News Desk