HabariSiasa

Danson Mwashako atoa onyo kwa shirika la kulinda na kuhifandi wanyama pori KWS kuondoa ndovu wanaozidi kuhangaisha wakaazi wa eneo bunge la Wundanyi

Mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako ame`toa onyo kwa shirika la kulinda na kuhifandi wanyama pori KWS kuondoa ndovu wanaozidi kuhangaisha wakaazi wa eneo hilo la sivyo wananchi wachukuwe hatua.

Mwashako anasema wakaazi wa eneo hilo wamepata hasara ya kutosha baada ya ndovu kuvamia mashamba sawa na kupasua matangi ya kuifadhia maji.

Haya yanajiri huku shuhuli za upanzi zikiendelea kaunti ya Taita Taveta huku wakulima wakihofia kuwa huenda mimea yao ikaharibiwa.