HabariMazingira

Wavuvi huko Mvureni DIANI walalamikia uhaba mkubwa wa samaki……

Wavuvi wanaohudumu kwenye ufuo wa bahari ya Mvureni wamelalamikia uhaba mkubwa wa samaki katika eneo la Diani kaunti ya Kwale.

Wakiongozwa na Ramadhan Suleiman, wavuvi hao wamedai kuwa idadi ya samaki katika bahari ya hindi imepungua kwa kiwango kikubwa.

Wameeleza kwamba hali hiyo imechangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa hatua ambayo imepelekea kupungua kwa mapato yao.

Wavuvi hao wamesema kuwa imekuwa vigumu kwao kupata wateja wa kununua samaki hali ambayo imewaathiri kiuchumi.

Sasa wanaitaka serikali ya kaunti ya Kwale kujitokeza na kuwapatia misaada baada ya shughuli zao kuathirika.

By Kwale Correspondent