HabariSiasa

Aliekua Mbunge Wa Kibwezi Magharibi Aaga Dunia………..

Aliyekuwa mbunge wa zamani wa eneo bunge la Kibwezi Magharibi, Kalembe Ndile ameaga dunia mapema leo katika Hospitali ya Nairobi.

Ndile ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 57, baada ya kuugua kwa muda mrefu akiuguza tatizo la ini.

Familia ya marehemu imethibitisha kifo chake huku Mwili wake ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee.

Mwendazake alihudumu kama waziri msaidizi wa wizara ya Utalii na Wanyamapori enzi za utawala wa rais mstaafu Mwai Kibaki