HabariNews

Watumizi wa barabara haswa madereva washauriwa kuwa na subra…….

Watumizi wa barabara hasa madereva wameshauriwa kuwa na subra wanapo tumia bara bara ili kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza na wandishi wa habari, msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema kwamba ajali nyingi zinatokana na watu kutokuwa na subra wanapotumia barabara jambo ambalo limechangia watu wengi kuaga duna.

Wakati huo huo kiongozi huyo amesisitiza  wananchi kuzingatia masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona, akisema kuwa ugonjwa huo ni hatari hasa kwa wale ambao hawezi kujikimu kimaisha.

Amesema hayo alipokuwa katika kaunti ya mombasa eneo bunge la Mvita alipokuwa akithathmini mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu wa Buxton.

By David Otieno