Habari

Naibu rais William Ruto Awahimiza wanaoshinikiza mswaada wa BBI kutupilia mbali mpango huo…………..

Naibu rais William Ruto amesema wale wanaoshinikiza katiba ifanyiwe marekebisho wanapaswa kutupilia mbali mpango huo, akisema maslahi ya taifa hili hayako katika mpango wa kufanyia marekebisho katiba kupitia BBI akisema BBI imekufa.

Akizungumza huko Kilifi Kusini akipokutana na wafanyibiashara wadodo wadogo kutoka wadi 35 za eneo bunge hilo, Ruto amesema wakati sasa ni wa kuzingatia kujenga uchumi wa nchi.

Wakati huo huo amesema mjadala unaopaswa kujadiliwa unapaswa uwe wa kuwawezesha wananchi haswa wafanyibiashara badala ya kuendeleza mijadala ya kutafutia watu mamlaka.

Kwa upande wake mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amewasuta wale ambao wanaingilia mipango ya hustler nation akisema sasa wamekosa la kufanya.

Aidha Jumwa amewasuta akiwataka wachague atakaye shindana na Ruto katika kinyanganyiro cha urais badala ya kupiga kelele zisizokuwa na msingi.

Wakati huo huo Ruto ametumia nafasi hiyo kuwatakia waislamu wote Eidul Adhha njema.