Habari

Serikali imejiandaa kwa ufunguzi wa shule muhula wa kwanza , asema waziri Magoha….

Waziri wa elimu Profesa George Magoha amesema kwamba serikali imejiandaa vya kutosha kwa ufunguzi wa shule kwa muhula wa kwanza juma lijalo baada ya kukamilisha malipo ya shilingi bilioni 17 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 59.5 kwa shule za upili za elimu ya mwaka uliopita.Akizungumza hapa Mombasa na washikadau wa sekta ya elimu, Magoha amesema tayari serikali imetenga fedha za muhula wa kwanza zitakazowasilishwa  shuleni punde tu mtambo wa IFMIS kuweza kufunguliwa.Na kuhusiana na maandalizi ya masomo ya CBC, Magoha amesema kwamba tayari asilimia 97 ya shule kote nchini zimepokea vitabu vya gredi ya tano huku akiongezea kwamba shule zote zinatarajiwa kupokea vitabu hivyo kufikia tarehe 26 july mwaka huu.Aidha Magoha ameongezea kwamba serikali imeweka mikakati kuona kwamba wanafunzi wote waliofanya mtihani wa darasa la nane wanajiunga na kidato cha kwanza kutimiza lengo la serikali kwamba asilimia mia moja ya wanafunzi wanavuka darasa la kwanza hadi jengine.

I

By Warda Ahmed