Habari

KEMSA yasema iko tayari kusambaza vifaa vya matibabu kote nchini…..

Mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu nchini KEMSA imesema iko tayari kusambaza vifaa vya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kote nchini punde tuu agizo hilo litakapotolewa na serikali.

Kaimu afisaa mkuu mtendaji wa KEMSA Edward Njoroge amesema mamlaka hiyo imebuni kamati maalumu ya kuhakikisha vifaa hivyo vinasambazwa kwenye kaunti zote 47.

Njoroge pia ametoa hakikisho kwamba KEMSA iko katika nafasi nzuri ya kushugulikia janga la corona kwa kusambaza vifaa muhimu kwa zaidi ya vituo 800 vya afya.

Haya yanajiri huku hospitali mbali mbali za umma humu nchini zikiwa zimejaa wagonjwa wa covid 19 hali ambayo imesababishwa na ongezeko la maambukizi ya corona.

Haya yanajiri huku viongozi wa kidini wakiwalaumu wanasiasa kwa ongezeko la maambukizi hayo kufuatia mikutano yao ya kisiasa.

Wamemtaka rais Kenyatta kuahirisha ziara yake eneo la magharibi ili kuzuia maambukizi zaidi.

By News Desk