Baraza la uanahabari nchini MCK limewaomba wanahabari pamoja na vyombo vya habari kuwa waangalifu hasa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 unapokaribia.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza hilo David Omwoyo amesema kuwa wanahabari wanapswa kuchukua hatua ya kutopeperusha matamshi ya viongozi na watu wanaoeneza matamshi ya chuki.
Omwoyo ameyasema haya wakati wa uzinduzi wa afisi za baraza hilo mjini Eldoret.
Kauli hii imeungwa mkono na naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Daniel Laboso ambaye amesema kwamba vyombo vya habari vinapswa kutumia nafasi yao kuelekeza umma kwa njia iliyo sawa.
BY PRESTON ALLAN