HabariMichezoNewsSports

Mashindano ya dunia kwenye mchezo wa riadha yaanza rasmi hii leo Nairobi….….

Mashindano ya Dunia kwenye mchezo wa riadha kwa vijana wasiozidi miaka 20 yameanza rasmi hii leo katika uwanja wa Moi Kasarani kaunti ya Nairobi.

Zaidi ya mataifa 100 yanashiriki mashindano haya yanayoendelea bila mashabiki chini ya taratibu zote  kukabili ugonjwa wa korona.

Hii leo asubuhi michezo ya kurusha jiwe,kisahani na mbio za mchujo mita 100 wavulana na wasichana imeanza kwa kishindo.

Hata hivyo wakenya wanasubiri mbio za mita 3000 kuruka maji na viunzi hatua ya mchujo mwendo wa saa kumi na moja.

Rais wa riadha duniani Sebastian Coe ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaohudhuria mashindano haya.

BY NEWS DESK