HabariNewsSiasa

Mudavadi aeleza matumaini ya kushinda urais uchaguzi mkuu ujao……

Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameelezea matumaini makubwa ya kukitwaa kiti cha urais ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Akizungumza katika makao makuu yake huko Nairobi, akihojiwa na radio moja humu nchini, Mudavadi amekariri kwamba ajenda yake kuu ni kufufua uchumi kupitia kupunguzwa kwa kodi na kuhakikisha kwamba wakenya wanasalia na fedha za kuwawezesha kukimu mahitaji yao.

Alipoulizwa iwapo hatachaguliwa kupeperusha bendera ya muungano wa ONE KENYE ALLIANCE OKA, kama atamuunga mkono yule atakayechaguliwa,Mudavadi alishikilia kwamba yeye ndio atakayechaguliwa kupeperusha bendera hiyo.

Kuhusu iwapo ana imani na tume ya IEBC kusimamia uchaguzi ujao, Mudavadi amesema kulingana na muda uliosalia hana budi ila kuiamini IEBC kusimamia uchaguzi huo.

BY NEWS DESK