HabariNews

Maafisa wa trafiki waonywa dhidi ya kuweka vizuizi barabarani…..

Maafisa wa trafiki wameonywa dhidi ya kukiuka agizo la awali la kuweka vizuizi vya barabarani kiholela.

Onyo hilo limetolewa na inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai baada ya mkutano na msaidizi wake wakiwemo makamanda wa kimaeneo.

Mutyambai alikuwa ametoa agizo hilo mwaka uliopita ambapo alipiga marufuku vizuizi vya kudumu ambavyo vinawekwa barabarani pasi na muongozo na vile vile kutoa muongozo wa jinsi ya kufanya hivyo haswa katika barabara kuu.

Hata hivyo watumizi wa barabara wamekuwa wakilalamikia kuendelea kupuuzwa kwa agizo hilo, katika maagizo hayo maafisa wa polisi pia wameonywa dhidi ya kuyazuia magari kwa muda mrefu.

Vizuizi vya barabarani vimekuwa vikitumika na baadhi ya maafisa wa trafiki wafisadi ili kuchukuwa hongo.

BY NEWS DESK