AfyaHabariNews

Mahakama Kuu imesitisha agizo la serikali linalotaka kila mkenya anayetafuta huduma za serikali apewe chanjo kamili ya Corona.

Mahakama kuu imesitisha kwa muda uamuzi wa serikali ya kitaifa ya kuhakikisha wakenya ambao hajawapokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona hawapati huduma kiserikali kuanzia tarehe 21 mwezi huu.
Uamuzi huo ambao umetolewa na jaji wa mahakama kuu Jaji Anthony Murima, umejiri kufuatia kukawia kwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi la kupinga agizo hilo.
Wakili Harrison Kinyanjui aliyewasilisha ombi mahakamani la kupinga uamuzi huo aidha amesisitiza kwamba hatua hiyo ya serikali ni kinyume cha sheria kwani kuchanjwa ni jambo la hiari.
Katika ombi lake wakili Kinyajui, amewashtaki makatibu wakuu katika wizara ya afya na usafiri, bodi ya kushughulikia maduka ya uuzaji dawa, inspekta mkuu wa polisi na mwanasheria mkuu.
Uamuzi wa jaji Mrima unajiri wakti ambapo baadhi ya maduka ya jumla pamoja na hoteli zikitoa taarifa kwamba hawatawahudumia raia ambao hawajachanjwa.
Haya yanajiri baada ya agizo la serikali la utoaji huduma kwa waliochanjwa pekee kutolewa na waziri wa afya humu Nchini Mutahi Kagwe ambalo linatarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi tarehe 21 mwezi huu.

BY NEWSDESK