HabariNewsSiasa

PWANI YAHOFIWA KUTOAPATA SAUTI MOJA YA KISIASA MWAKA 2022.

Magavana Salim Mvurya wa kaunti ya Kwale, Hassan Joho wa kaunti ya Mombasa na Amason Kingi wa kaunti ya Kilifi wamechukua mielekeo tofauti kuhusu uchaguzi ujao, hasa wa urais watakapo kamilisha vipindi vyao vya pili vya uchaguzi.
Mvurya ameegemea upande wa Naibu Rais William Ruto, Joho akiunga mkono azimio la Kinara wa Cha ODM, Raila Odinga huku Kingi akiashiria kumuunga mkono Odinga kwa urais ingawa amesema atapigia debe wanasiasa watakao wania viti vingine kupitia Chama cha Pamoja African Alliance PAA.
Misimamo hii mikali imesababisha baadhi ya viongozi wa kijamii na wanasiasa kuonya kwamba Pwani itakuwa hatarini na kukosa nafasi nzuri katika meza ya serikali ya kitaifa baada ya uchaguzi ujao.
Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa muungano wa kitamaduni wa kaya za Wamijikenda Malindi, Joseph Karisa Mwarandu, ni kwamba wazee wa jamii za Wamijikenda sasa wamesisitiza kuwa ni sharti watatu hao wazike tofauti zao kwa minajili ya kuwatumikia Wapwani.
Aidha wameongeza kwamba Pwani haitapata sauti moja kisiasa mwaka 2022 iwapo watatu hao watakuwa bado wametengana.

BY NEWSDESK