HabariNews

Kamati ya Kitaifa ya Utekelezaji wa maendeleo NDITC inakagua Ujenzi mradi wa Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala unaoendelea katika eneo la Vipingo, Kaunti ya Kilifi.

Kamati ya Kitaifa ya Utekelezaji wa maendeleo NDITC inakagua
Ujenzi mradi wa Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala unaoendelea
katika eneo la Vipingo, Kaunti ya Kilifi. Mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2013, umechukua
mda mrefu bila kukamilika licha ya kutengewa fedha za kutosha
huku kufikia Agosti mwaka uliopita, ujenzi huo ulikuwa umefikia
asilimia 60 pekee licha ya kutarajiwa kukamilika Mwezi Juni mwaka
2019. Kufikia Mwezi Agosti mwaka uliopita, Mradi huo ulikuwa umetumia
Zaidi ya shilingi Bilioni 8, mbali na shilingi Bilioni 4.9 ambazo
zilikuwa zimetengewa na haya ni kwa mujibu wa kamati ya
utekelezaji katika Bunge la Kitaifa. Itakumbukwa kwamba tarehe 29 Mwezi Sepemba mwaka 2020,
Kamati ya uwekezaji katika Bunge la Kitaifa ilimtaka Waziri wa
Utalii Najib Balala kufika mbele yake kujibu maswali kuhusu
ubadhirifu wa fedha za mradi huo.