HabariNews

Makatibu wa wizara mbalimbali nchini wamekita kambi katika kaunti ya Kwale kufanya ukaguzi wa miradi inayoendelezwa na serikali.

Makatibu wa wizara mbalimbali nchini wamekita kambi katika
kaunti ya Kwale kufanya ukaguzi wa miradi inayoendelezwa na
serikali. Baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kaunti
hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Kinango-Kwale, ujezi wa
mabweni katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa tawi la
Kwale na ujezi wa bwawa la Mwache. Makatibu hao wakiongozwa na katibu wa kawi, Godwin Kihalagwa
wamegadhamishwa na kujikokota kwa ujenzi wa barabara ya
Kinango-Kwale, huku kandarasi ya bara bara hiyo yenye urefu wa
kilomita 29 itakayo gharimu bilioni 3 ilitolewa mwaka jana mwezi
Disemba na kufikia sasa ujezi wake haujaanza.