HabariNews

Maafisa wa usalama wameitaja Kaunti ya Kwale kuwa chimbuko la visa vya ugaidi katika Ukanda wa Pwani.

Maafisa wa usalama wameitaja Kaunti ya Kwale kuwa chimbuko la visa vya ugaidi katika Ukanda wa Pwani, huku machifu wawili wakienda mafichoni baada ya kutishiwa maisha yao.
Mshirikishi wa usalama katika Ukanda wa Pwani John Elung’ata, amesema kwamba Kaunti hiyo imebainika kuwa na vituo viwili vya magaidi ambapo watu hufunzwa itikadi kali kabla kwenda kutekeleza mashambulio humu nchini na nje ya nchi.
Elung’ata aidha amesema kwamba Kaunti hiyo imegeuka kuwa ngome ya kusafirisha watu wenye itikadi za kigaidi nchini Msumbiji na Somalia, kwani wengi wa wale wanaokamatwa katika nchi hizo ni wazaliwa wa Kwale.
Mshirikishi huyo ametoa tahadhari kwa vijana dhidi ya kujihusisha na makundi ya kigaidi kwamba Serikali iko sako kwa bako nao.