Mkurugenzi wa elimu ukanda wa pwani Adan Hussein ameagiza shule ya kibinafsi ya Gremon eneo la Bamburi katika kaunti ya Mombasa kufungwa.
Kauli yake inajiri baada ya madai ya mkurugenzi wa shule hiyo kumuadhibu vibaya mwanafunzi mmoja wa darasa la saba aliyepata majeraha mabaya ambapo anaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani-Coast General.
Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Mombasa amesema wameanzisha uchunguzi wa kina ambapo ataweka bayana ripoti kamili kuhusu kisa hicho na hatma ya shule hiyo hapo baadaye baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
BY EDITORIAL DESK