Uncategorized

Wakimbizi kutoka nchi nyingine watakiwa kutafuta vibali.

Katibu katika shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Allan Nyange ametoa wito kwa wakimbizi kutoka nchi nyingine kuhakikisha kuwa wanatafuta vibali vinavyowaruhusu kuwa humu nchini ili waepuke kukabiliwa na makosa ya kisheria.
Kauli yake inajiri baada ya wakimbizi kadhaa hususan kutoka nchi za Ethiopia na somalia kukamatwa na maafisa wa polisi kwa shutuma za kuwa humu nchini kinyume na sheria .
Hata hivyo,Nyange amerai wananchi kuwa macho na kuripoti mtu yeyote wanayetilia shaka mienendo yake.