HabariNews

Takriban Wapemba elfu 4 wanaoishi kaunti ya Kwale na nwenye asili ya taifa jirani la Tanzania wanahangaika kufuatia ukosefu wa vitambulisho vya kitaifa.

Takriban Wapemba elfu 4 wanaoishi kaunti ya Kwale na nwenye asili ya taifa jirani la Tanzania wanahangaika kufuatia ukosefu wa vitambulisho vya kitaifa.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Hamis Makame, jamii hiyo imeshinikiza serikali kupitia wizara ya usalama nchini kuharakisha mpango wa kuwapa vitambulisho hivyo.
Aidha, jamii hiyo inayodai uraia wa Kenya inadai kwamba haiwezi kumiliki kitu chochote wala kupata huduma muhimu kutoka serikalini.
Hata hivyo, afisa wa shirika la kitaifa la kutetea haki za kibinadamu la (KHRC) Robert Waweru ameahidi kushughulikia suala hilo ili kuhakikisha jamii hiyo inapata stakabadhi hiyo muhimu.
Haya yanajiri baada ya jamii ya Wamakonde ambalo chimbuko lake ni Musumbiji kupewa vitambulisho vya kitaifa na serikali ya kitaifa.
Mwisho