HabariNewsSiasa

Bodi ya mamlaka ya ununuzi na usambazaji dawa pamoja na vifa aa vya kimatibabu KEMSA yajitetea kufuatia ripoti kuhusu kupotea kwa vifaa vya zaidi ya shilingi milioni 10.

Bodi ya mamlaka ya ununuzi na usambazaji dawa pamoja na vifa aa vya kimatibabu KEMSA imejitetea kufuatia ripoti kuhusu kupotea kwa vifaa vya zaidi ya shilingi milioni 10.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mary Mwadime amesema hakuna sakata ambayo imeripotiwa chini ya uongozi wake kwani utepetevu katika KEMSA uliripotiwa kati ya January mwaka wa 2018 na Aprili mwaka wa 2021.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Mwadime amesema kuwa mabadiliko makuu yamefanyika katika KEMSA tangu achukue usukani akiongeza kuwa miongoni mwa mafanikio ni usambazaji wa vifaa vya kimatibabu vya thamani ya shilingi milioni 35.84 vilivyosambazwa katika vituo vya afya 11,500 kote nchini.