HabariMombasaNewsSiasa

Naibu wa rais William Ruto aihakikishia jamii ya wamijikenda na Pwani kwa Ujumla kufanya kazi nao kwa karibu atakaposhinda uchaguzi mkuu ujao.

Naibu wa rais William Ruto amewahakikishia jamii ya wamijikenda na Pwani kwa Ujumla kufanya kazi nao kwa karibu atakaposhinda uchaguzi mkuu ujao.
Ruto amesema kuwa yuko tayari kuwapatia nafasi zaidi za uaziri kutokana na ufuasi anaondelea kupata kutoka eneo hilo.
Kauli ya Ruto inajiri baada ya mkutano na wanachama cha chama cha Kadu Asili na baraza la wazee wa Amidzi kutoka Pwani mapema wiki hii.
Mkutano huo pia ulishuhudia ushirikiano wa aliyekuwa muaniaji wa kiti cha Ugavana kaunti ya Kilifi kupitia tiketi ya chama cha Kadu Asili Emanuel Nzai kuwa naibu wa mwaniaji wa Ugavana wa UDA Aisha Jumwa.