HabariNewsSiasa

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inatarajiwa kufika mbele ya kamati ya seneti ya sheria.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inatarajiwa kufika mbele ya kamati ya seneti ya sheria ili kuhojiwa kuhusu maandalizi yake kwa ajili ya uchaguzi wa agosti 9.
Maswala muhimu yanayotarajiwa kuibuka wakati wa kamati hiyo ni pamoja na ukaguzi wa sajili ya wapiga kura.
Wiki jana IEBC ilisema imeipa kampuni ya KPMG zabuni hiyo.
Ikiwa imesalia miezi 4 kabla ya uchaguzi mkuu, Mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati alieleza matumaini kwamba shughuli hiyo itakamilika kwa wakati akipuuza madai kwamba mda ulikuwa umekwisha akisema makataa ya sajili kufanyiwa ukaguzi miezi 6 kabla ya uchaguzi mkuu yalikuwa yatumike tu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.