HabariNews

MABADILIKO YA MILA NA TAMADUNI YACHANGIA PAKUBWA ONGEZEKO LA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA PWANI YASEMA NACADA.

Mamlaka ya kukabili matumizi ya dawa za kulevya nchini inasema NACADA mabadiliko ya mila na tamadumu yamechangia pakubwa ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya hasa hapa eneo la pwani.
Akizungumza ofisini mwake Mkurugenzi wa NACADA nchini Farida Toll amesema hapo nyuma jamii hasa mababu walikuwa na hulka ya kuelekeza vijana na wajukuu wao kuhusu maadili mema.
Farida anasema muingilio wa tabia za mataifa ya nje vimevuruga hali ya maisha ya familia nyingi na kuchangia familia kusahau majukumu yao, jambo linalochangia vijana kutumia dawa za kulevya na kujiingiza kwenye visa vya uhalifu.
Wakati huo huo ameshauri familia ambazo vijana wao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya kujitolea na kuwapeleka katika vituo vya kurekebishia tabia ili kusaidika.

BY EDITORIAL TEAM