HabariSiasa

WAGOMBEA SITA WA KITI CHA UGAVANA KAUNTI YA KWALE WAIDHINISHWA NA IEBC.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchni IEBC imewaidhinisha wagombea sita wa kiti cha ugavana kaunti ya kwale.
Kwa hivi punde kuidhinishwa ni spika wa bunge la kaunti hiyo Sammy Ruwa anayewania kama mgombea huru na Chai lung’anzi anayewania kwa tiketi ya chama cha PAA. ambaye ameahidi kulipa swala la maji kipao mbele naye Ruwa akiahidi kualika wawekezaji ili kuwekeza katika viwanda na kuboresha biashara kaunti hiyo.
Zaidi ya wapiga kura laki mbili na elfu themanini wataamua gavana wao ni nani kaunti ya kwale kati ya wagombea hao ambao kando na Sammy Ruwe na Chai Lung’anzi wengine ni Fatuma achani wa UDA, proffesa Hamadi Boga Wa ODM ,Ali Chirau Mwakwere wa chama cha Wiper na Gereza Dena wa chama cha KANU huku maafisa wa tume hiyo wakitaka wanasiasa walioidhinishwa kuendesha kampeni zao kwa njia ya amani.

>> News Desk.