HabariMombasa

KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI LAENDELA MOMBASA KUTAFUTA NJIA MBADALA YA USALAMA BARABARANI ILI KUPUNGUZA VISA VYA AJALI.

Kongamano la usalama barabarani linaendelea hapa kaunti ya Mombasa linalowaleta pamoja wadau kutoka sekta ya uchukuzi kujadili jinsi ya kupunguza visa vya ajali wanavyodai kuongezeka siku za hivi karibuni.
Kulingana na Samuel Msumba mmoja wa maafisa wa NTSA akizungumza na waandishi wa habari amesema Kongamano hilo ni lakujaribu kutafuta njia mbadala na kuboresha usalama barabarani ili kupunguza visa vya Ajali.
Aidha amewalaumu madereva wengi kutokuwa makini na kufwata kanuni za barabarani hali ambayo imepelekea kutokea kwa ajali ambazo zingeepukika.

>> News Desk