HabariSiasa

Marekani yaipongeza IEBC kwa kukamilisha shughuli ya kuwaidhinisha wagombea.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Athony Blinken ameipongeza tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa kukamilisha shughuli ya kuwaidhinisha wagombea mbali mbali katika uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Katika taarifa yake leo hii Waziri huyo amesema Marekani inaunga mkono uchaguzi huru na haki.
Kupitia mtandao wake wa Twitter Blinken amesema Marekani inatarajia uchaguzi mkuu hapa nchini kuwa huru na haki.
Taarifa hii inajiri siku 3 baada ya tume ya IEBC kukamilisha zoezi la kuwaidhinisha wawaniaji wa viti mbali mbali vya kisiasa.

>> News Desk…