Habari

Oparesheni ya kunasa magari yanayokiuka sheria za barabarani kuanzishwa.

Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutiambai ameagiza kufanyike oparesheni ya kunasa magari yanayokiuka sheria za barabarani sambamba na madereva wa magari hayo.
Hii ni kulingana na taarifa iliyochapishwa katika kurasa za mtandao wa kijamii wa idara ya polisi oparesheni hiyo imesababishwa na ongezeko la ajali barabarani.
Takwimu zinaonyesha katika kipindi cha miezi 6 ya kwanza mwaka huu ajali zimeongezeka kwa kiwango cha asilimia 9.3 ikilinganishwa na kipindi sawia mwaka jana.

>> News Desk…