Habari

Famila moja kisiwani Amu inataka haki kwa binti yao.

Famila moja kisiwani Amu inataka haki kwa binti yao wa umri wa miaka 15 anayedaiwa kunajisiwa kisha kutupwa katika ufuo wa bahari huko Shella akiwa amefugwa mikono, miguu na mdomo kabla ya kuokolewa na polisi.
Msichana huyo ambaye jina lake tumelibana na ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule moja ya msingi, alitekwa nyara na wanaume watatu waliomvamia asubuhi ya saa kumi na mbili alipokuwa akijitayarisha kuenda shuleni.
Babake msichana huyo amesema alipokea simu kwamba alikuwa akihitajika katika hospitali kuu ya rufaa ya King Fahad na alipofika hospitalini akamkuta bintiye akiwa amepoteza fahamu.
Kulingana na Msichana alivamiwa na wanaume watatu waliomdunga sindano mbili shingoni japo akawatambua wawili kati yao kabla ya kupoteza fahamu.
Muathiriwa amepata fahamu baada ya takribanisaa 30, huku kamishena wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia akiwataka wazazi kuwachunga watoto wao.

>> News Desk.