HabariMombasaSiasa

Naibu gavana Kaunti ya Mombasa Dr. William Kingi anasema amekuwa na changamoto kumfikia gavana Ali Hassan Joho tangu apokonywe magari yake pamoja na walinzi wake.

Naibu gavana Kaunti ya Mombasa Dr. William Kingi anasema amekuwa na changamoto kumfikia gavana Ali Hassan Joho tangu apokonywe magari yake pamoja na walinzi wake.
Kingi ambaye anawania wadhifa wa ugavana kupitia chama cha PAA, anasema hafahamu kinachoendelea kwa kuwa hajawahi kutofautiana na gavana Joho.
Akizungumza katika kipindi cha Sauti Asubuhi hapa Sauti ya Pwani, Kingi amesema anahisi huenda sintofahamu anakumbana nazo zinachangiwa na msimamo wake wa kisiasa.
Vile vile Kingi amesema wakaazi wa Mombasa wanahitaji mabadiliko kutokana na mapungufu ambayo yamechangiwa na viongozi walio madarakani na ambao wanaondoka kwa sasa.

>>News Desk