HabariSiasa

Wanasiasa wanaotumia semi za uchochezi Kaunti Kilifi Kuchukuliwa hatua za kisheria………..

Shirika la kutetea haki za kibinadam la KECOSCE katika kaunti ya Kilifi limesema litashirikiana kwa ukaribu na idara ya usalama ili kuwachukulia hatua wanasiasa wanaotumia semi za uchochezi katika kampeni zao.
Afisa wa mipango wa shirika hilo Kibwana Hassan, anasema shirika hilo pamoja na mashirika mengine ya kijamii yanafuatilia kwa ukaribu siasa zinazoendelea ili kubaini wanasiasa hao.
Hassan amedokeza kuwa mashirika ya kijamii hayatasita kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa walio na nia ya uchochezi na kuvuruga amani katika eneo hili.

>> News Desk…