HabariSiasa

Chama cha Wiper chamemtetea aliyekuwa gavana wa Nairobi mike Sonko.

Chama cha Wiper kimemtetea aliyekuwa gavana wa Nairobi mike Sonko ambaye amezuliwa na tume ya uchaguzi kuwania wadhfa wa ugavana kaunti ya Mombasa.
Wiper imewasilisha lalama dhidi ya Mwenyekiti ya IEBC Wafula Chebukati kwa jopo la kutatua mizozo ya kisiasa nchini.
Kiongozi wa chama Hicho Kalonzo Musyoka anadai Sonko anakandamizwa na IEBC kwa lengo la kuzuia kuwahudumia wakaazi wa Mombasa.
Amesema hayo katika mahakama ya Milimani Jijini Nairobi akiwa ameandamana na Sonko Pamoja na viongozi wengine wa chama hicho, ambapo jopo lililoteuliwa na IEBC linasikiliza lalama zilizoibuliwa na wagombea mbali mbali waliozuiliwa kugombea.
Kalonzo ametaka malalamishi ya wiper Pamoja na ya Sonko kushughulikiwa kwa haraka.

>> News Desk