HabariMombasa

Wakaazi wa eneo la Pwani ya Kenya walalamikia kupanda kwa gharama ya Maisha.

Wakaazi hapa Pwani wanalalamikia kupanda kwa gharama ya Maisha wengi wakisema wameshindwa kukidhi mahitaji ya kimsingi ikiwemo kununua chakula, matibabu na kulipia wanao karo.
Waakzi waliozungumza na Sauti ya pwani wameshinikiza serikali kuchukua hatua za haraka kutatua hali hii, ambayo wanasema huenda ikawa mbaya hat ana zaidi siku zijazo.
Hivi majuzi mamlaka ya kudhibiti bei za mafuta EPRA ilitangaza kuongezeka kwa bei ya mafuta katika aina zote za mafuta kwa shilingi 9.
Baadhi wanasema hali hiyo huenda ikachangia kuongezeka kwa visa vya uhalifu.

>> News Desk…