HabariSiasa

Waziri wa usalama wa kitaifa Daktari Fred Matiang’i ahakikishia wakenya uchaguzi huru na haki.

Waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiang’I amesema uchaguzi mkuu wa agosti 9 utakuwa huru na Haki.
Akizungumza baada ya mkutano na mabalozi wa kenya katika mataifa mbali mbalia, Matiang’I amesistiza kuwa serikali kamwe haitafunga mitandao wakati huo.
Amesema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha changamoto zote zinazoweza kuathiri shughuli ya uchaguzi kama vile utovu wa usalama, kununuliwa kwa wapiga kura na kukabili jumbe za chuki kupitia mitandao ya kijamii zinashughulikiwa.
Waziri huyo vile vile amesema kenya haitarajii changamoto zozote zinazoweza kuathiri uhusiano baina yake na mataifa mengine.

>> News Desk…