HabariKimataifa

KRA IMERIPOTI ONGEZEKO LA MAPATO YA USHURU.

Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini (KRA) imeripoti ongezeko la mapato ya ushuru kwa muda wa mwaka mmoja kufuatia kujumuishwa kwa mpaka wa Kenya na Tanzania katika kaunti ya Kwale.

Afisa wa mamlaka hiyo katika eneo la Pwani John Changole amesema kuwa kiwango cha ushuru kimeimarika kwa zaidi ya shilingi milioni 700 kila mwezi tangu kujumuishwa kwa mpaka huo.

Changole amesema kuwa mabadiliko hayo katika mpaka wa Lungalunga-Horohoro pia yamechangia shughuli za usafirishaji wa bidhaa baina ya Kenya na Tanzania kimeimarika.

Kwa upande wake dereva wa basi la kubeba abiria Sultan Abushiri amesema kuwa shughuli za ukaguzi wa pasi za usafiri zimerahishwa katika mpaka huo.

Abushiri amedokeza kwamba sasa shughuli hiyo inachukua muda mfupi ikilinganishwa na hapo nyuma ambapo abiria walilazimika kusubiri kwa saa mbili.

>> News Desk…