Habari

NAIBU RAIS WILLIAM RUTO AMEFANYA KIKAO NA WALEMAVU.

Mpeperusha bendera ya urais wa muungano wa Kenya Kwanza William Ruto amefanya kikao na watu wenye ulemavu jijini Nairobi, ili kupata taswira kamili ya masuala wanayotaka yashughulikiwe na serikali yake endapo atatwaa uongozi wan chi.

Ruto amesema kuwa mapendekezo atakayokabidhiwa na watu hao yanajumuishwa kwenye manifesto yake ambayo ameratibiwa kuizindua tarehe 30 mwezi huu wa Juni.

Aidha seneta maalum Isaac Mwaura amesema kuwa watu wenye mahitaji maalum wamekuwa wakipitia changamoto za kubaguliwa katika jamii hali ambayo imewafanya wengi kujificha na kushindwa kutetea haki zao.

>> News Desk…