Habari

Kituo cha pili cha kuegesha makasha katika bandari ya Mombasa sasa kiko tayari.

Kituo cha pili cha kuegesha makasha katika bandari ya Mombasa kimekamilika na sasa kiko tayari kuanza shughuli za bandari. Kituo hicho chenye urefu wa mita mia tatu kitasaidia kumaliza msongamano wa makasha bandarini. Kwa mujibu wa wakurugenzi katika halmashauri ya bandari nchini (KPA) bandari hiyo sasa inadhamiria kuongeza idadi ya treni za makasha ambazo hutoka Mombasa kwenda Naivasha kila siku hadi kumi na tano. Aidha kituo hicho pia kitasaidia katika kuongeza nafasi za ajira kwa vijana katika bandari hiyo, baada ya shirika la reli humu nchini kutangaza kuwa limeagiza mabehewa zaidi kuongezea kwa yale ambayo yapo nchini huku shughuli za ukarabati wa reli eneo la Taita Taveta zikishinikizwa kuanza.

>> News Desk…