Habari

Haki Yetu limelaumu taasisi huru za kiserikali kwa madai ya kushindwa kuwakabili viongozi wa kisiasa wasiokuwa na maadili.

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Yetu limelaumu taasisi huru za kiserikali kwa madai ya kushindwa kuwakabili viongozi wa kisiasa wasiokuwa na maadili.

Afisa wa miradi katika shirika hilo Jamal Abdallah anadai kuwa taasisi hizo zimeshindwa kuwazuia wanasiasa wenye maswali ya ukosefu wa uadilifu kupigania nyadhifa za uongozi.

Akizungumza katika eneo la Matuga, Abdallah amesema tume ya uchaguzi nchini (IEBC) na tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC) zimeingiliwa kisiasa na kuathiri utendakazi wao.

Abdallah amewaonya wakenya dhidi ya kuwachagua viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi, mauaji na stakabadhi ghushi za masomo.

>> Editorial Desk…