HabariNewsSiasa

Dini na utamaduni vimetajwa kumkandamiza mwanamke katika kaunti ya Kwale.

Dini na utamaduni vimetajwa kumkandamiza mwanamke katika nafasi za ajira na uongozi ndani ya kaunti ya Kwale kama njia ya kumnyamazisha kutofikia malengo yake.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la HURIA Yusuf Lule akizungumza huko Ukunda kaunti ya Kwale wakati wa kuzindua mpango wa utekelezaji wa usalama na amani (ACTION PLAN), amesema kuwa watu wanavitumia vigezo hivyo kuwavunja moyo wanawake wanao wania na kupigania nyadhfa za uongozi na hata masuala ya kupambana usalama na amani.
Kwa upande wake kiongozi wa kamati ya usalama nyanjani, Mwanakombo Jerumani amesema kuwa watu wanatumia utamaduni uliopitwa na wakati unaomgandamiza mwanamke hivyo basi ipo haja ya kufuata tamaduni mambo-leo ili kuwezesha wanaoweza kuongoza kuwapa nafasi kando na kutumia tamaduni potuvu kwa kumkata sauti mwanamke kutoweza kuzungumza.
Aidha Jerumani amewataka wakaazi wa Kwale na wakenya kwa ujumla kutotumia mila potovu na kugeuza baadhi ya aya katika vitabu vitakatifu kumkandamiza mwanamke.

>>> By Editorial Desk